The best prize life has to offer is not a chance to work hard and be something in the community. It is the perfume of God that resides within you.
Enock Maregesi
Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.
change children freedom
Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine.
truth
Watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi. Wanaheshimu nguvu ya matendo yako.
attitude
Ukitaka kuleta mabadiliko katika dunia huna budi kubadilika wewe kwanza. Ukibadilika ukawa mwema katika jamii yako umeleta mabadiliko katika dunia.
change
Kujiingiza katika madawa ni matokeo ya maisha. Hatutumii madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya ni sisi wenyewe; tunahitaji kusaidiwa.
drugs
Situmii madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya ni mimi mwenyewe; nahitaji kusaidiwa!
Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi.
government pressure law
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine.
selfishness hell suicide
Watu wanapokuwa katika migogoro maisha yao hutakiwa kurahisishwa. Kuna ukingo mwembamba kati ya uzima na wazimu.
inspirational-attitude
Mojawapo ya misingi ya ujasusi ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya unachojua, usichojua na unachofikiria. Unaweza kusema unajua wakati hujui. Maamuzi yasiyo sahihi ya kijasusi huweza kuiletea tume madhara makubwa.
intelligence
Iwapo kila mtu atamheshimu mwenzake kama anavyojiheshimu mwenyewe; tunaweza kuishi mbinguni duniani.. Lakini kwanza tuwe na maarifa binafsi.
peace inspirational
peace
Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.
poverty wealth poor rich
Migogoro inatokea kwa sababu watu wameshindwa kuheshimiana. Ukijiheshimu na ukaheshimu wengine; utaacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta, wakati ukiingia.
inspirational respect
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.
life sacrifice
Showing 1 to 15 of 22 results
You must log in to post a comment.
There are no comments yet.